2 Samweli 15:9
2 Samuel 15:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mfalme akamwambia, “Enenda kwa amani.” Hivyo akaenda Hebroni.
2 Samuel 15:9 in English
2 Samuel 15:9 · Berean Standard Bible
“Go in peace,” said the king. So Absalom got up and went to Hebron.
Context
7Mnamo mwisho wa mwaka wa nne, Absalomu akamwambia mfalme, “Naomba unipe ruhusa niende Hebroni nikatimize nadhiri niliyomwekea Bwana. 8Wakati mtumishi wako alipokuwa huko Geshuri katika nchi ya Aramu, niliweka nadhiri hii, ‘Ikiwa Bwana atanirudisha Yerusalemu, nitamwabudu Bwana huko Hebroni.’ ” 9Mfalme akamwambia, “Enenda kwa amani.” Hivyo akaenda Hebroni. 10Kisha Absalomu akatuma wajumbe kwa siri katika makabila yote ya Israeli, kusema, “Mara mtakaposikia sauti ya tarumbeta basi semeni, ‘Absalomu ni mfalme huko Hebroni.’ ” 11Watu mia mbili kutoka Yerusalemu walikuwa wamefuatana na Absalomu. Walikuwa wamealikwa kama wageni nao walikwenda kwa nia njema, pasipo kujua lolote.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.