Native Bible

2 Samuel 15:33 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Daudi akamwambia, “Kama ukienda pamoja nami, utakuwa mzigo kwangu.

2 Samuel 15:33 in English

2 Samuel 15:33 · Berean Standard Bible

David said to him, “If you go on with me, you will be a burden to me.

Context

31Basi Daudi alikuwa ameambiwa, “Ahithofeli alikuwa miongoni mwa washiriki wa shauri baya la Absalomu.” Ndipo Daudi akaomba, akisema, “Ee Bwana, geuza shauri la Ahithofeli kuwa ujinga.” 32Daudi alipofika kwenye kilele cha mlima, mahali ambapo watu walikuwa wamezoea kumwabudu Mungu, Hushai, Mwariki, alikuwako huko kumlaki, joho lake likiwa limeraruka na mavumbi kichwani mwake. 33Daudi akamwambia, “Kama ukienda pamoja nami, utakuwa mzigo kwangu. 34Lakini ikiwa utarudi mjini na kumwambia Absalomu, ‘Nitakuwa mtumishi wako, ee mfalme; nilikuwa mtumishi wa baba yako wakati uliopita, lakini sasa nitakuwa mtumishi wako,’ basi utaweza kunisaidia kwa kupinga shauri la Ahithofeli. 35Je, makuhani Sadoki na Abiathari hawatakuwa pamoja nawe? Waambie lolote utakalosikia katika jumba la mfalme.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.