2 Wafalme 4:33
2 Kings 4:33 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Akaingia ndani, akajifungia yeye na yule mtoto, akamwomba Bwana.
2 Kings 4:33 in English
2 Kings 4:33 · Berean Standard Bible
So he went in, closed the door behind the two of them, and prayed to the LORD.
Context
31Gehazi akatangulia mbele na kuilaza fimbo juu ya uso wa mtoto, lakini hapakuwa na sauti wala itikio. Hivyo Gehazi akarudi kukutana na Elisha, na kumwambia, “Mtoto hajaamka.” 32Elisha alipofika kwenye ile nyumba, mtoto alikuwa amelala juu ya kitanda chake angali amekufa. 33Akaingia ndani, akajifungia yeye na yule mtoto, akamwomba Bwana. 34Kisha akapanda kitandani, akalala juu ya yule mtoto, mdomo wake juu ya mdomo wa mtoto, macho yake juu ya macho ya mtoto, mikono yake juu ya mikono ya mtoto. Naye alipojinyoosha juu yake, mwili wa mtoto ukapata joto. 35Elisha akajiondoa juu yake na kuanza kutembeatembea ndani ya chumba, kisha akarudi tena kitandani na kujinyoosha tena juu ya mtoto mara nyingine. Mtoto akapiga chafya mara saba, akafungua macho yake.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.