2 Wafalme 4:18
2 Kings 4:18 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mtoto akakua, naye siku moja akamwendea baba yake, ambaye alikuwa pamoja na wavunaji.
2 Kings 4:18 in English
2 Kings 4:18 · Berean Standard Bible
And the child grew, and one day he went out to his father, who was with the harvesters.
Context
16Elisha akamwambia, “Mwaka ujao, wakati kama huu utabeba mwana mikononi mwako.”
Yule mama akapinga, akasema, “La hasha, bwana wangu, usimpotoshe mtumishi wako, ee mtu wa Mungu!” 17Lakini yule mwanamke akapata mimba, na mwaka uliofuata wakati kama ule ule akamzaa mwana, kama vile Elisha alivyokuwa amemwambia. 18Mtoto akakua, naye siku moja akamwendea baba yake, ambaye alikuwa pamoja na wavunaji. 19Akamwambia baba yake, “Kichwa changu! Kichwa changu!”
Baba yake akamwambia mtumishi, “Mchukue umpeleke kwa mama yake.” 20Baada ya mtumishi kumbeba na kumpeleka kwa mama yake, mtoto akaketi mapajani mwa mama yake mpaka adhuhuri, kisha akafa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.