2 Wafalme 3:1
2 Kings 3:1 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Yehoramu* mwana wa Ahabu akawa mfalme wa Israeli katika Samaria mwaka wa kumi na nane wa utawala wa Yehoshafati mfalme wa Yuda, naye akatawala kwa miaka kumi na miwili.
2 Kings 3:1 in English
2 Kings 3:1 · Berean Standard Bible
In the eighteenth year of Jehoshaphat’s reign over Judah, Jehoram * son of Ahab became king of Israel, and he reigned in Samaria twelve years.
Context
1Yehoramu* mwana wa Ahabu akawa mfalme wa Israeli katika Samaria mwaka wa kumi na nane wa utawala wa Yehoshafati mfalme wa Yuda, naye akatawala kwa miaka kumi na miwili. 2Akafanya maovu machoni pa Bwana, lakini sio kama baba yake na mama yake walivyokuwa wamefanya. Akaondoa nguzo ya ibada ya Baali ambayo baba yake alikuwa ameitengeneza. 3Hata hivyo akashikamana na dhambi za Yeroboamu mwana wa Nebati, ambazo alisababisha Israeli kuzitenda, wala hakuziacha.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.