2 Wafalme 25:17
2 Kings 25:17 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kila nguzo ilikuwa na urefu wa dhiraa kumi na nane.* Sehemu ya shaba juu ya nguzo moja ilikuwa na urefu wa dhiraa tatu* na ilikuwa imepambwa kwa wavu na makomamanga ya shaba kuizunguka kote. Ile nguzo nyingine pamoja na wavu wake ilifanana na hiyo ya kwanza.
2 Kings 25:17 in English
2 Kings 25:17 · Berean Standard Bible
Each pillar was eighteen cubits tall.* The bronze capital atop one pillar was three cubits high,* with a network of bronze pomegranates all around. The second pillar, with its network, was similar.
Context
15Jemadari wa askari walinzi wa mfalme akachukua vile vyetezo na yale mabakuli ya kunyunyizia, vitu vyote vile vilivyokuwa vimetengenezwa kwa dhahabu safi au fedha. 16Shaba iliyotokana na zile nguzo mbili, ile Bahari na vile vishikilio vilivyohamishika, ambavyo Solomoni alikuwa ametengeneza kwa ajili ya Hekalu la Bwana, ilikuwa na uzito usioweza kupimika. 17Kila nguzo ilikuwa na urefu wa dhiraa kumi na nane.* Sehemu ya shaba juu ya nguzo moja ilikuwa na urefu wa dhiraa tatu* na ilikuwa imepambwa kwa wavu na makomamanga ya shaba kuizunguka kote. Ile nguzo nyingine pamoja na wavu wake ilifanana na hiyo ya kwanza. 18Yule jemadari wa askari walinzi akawachukua kama wafungwa Seraya kuhani mkuu, kuhani Sefania aliyefuata kwa cheo, na mabawabu watatu. 19Miongoni mwa wale watu waliokuwa wamesalia katika mji, alimchukua afisa kiongozi wa wapiganaji, na washauri watano wa mfalme. Akamchukua pia mwandishi aliyesimamia uandikishaji wa watu wa nchi, pamoja na watu wake sitini waliopatikana ndani ya mji.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.