Native Bible

2 Kings 23:32 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Akafanya maovu machoni mwa Bwana, kama baba zake walivyofanya.

2 Kings 23:32 in English

2 Kings 23:32 · Berean Standard Bible

And he did evil in the sight of the LORD, just as his fathers had done.

Context

30Watumishi wa Yosia wakauleta mwili wake katika gari la vita kutoka Megido hadi Yerusalemu, wakamzika kwenye kaburi lake mwenyewe. Nao watu wa nchi wakamchukua Yehoahazi mwana wa Yosia, wakamtia mafuta na kumfanya mfalme mahali pa baba yake. 31Yehoahazi alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitatu alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu kwa miezi mitatu. Jina la mama yake aliitwa Hamutali binti Yeremia kutoka Libna. 32Akafanya maovu machoni mwa Bwana, kama baba zake walivyofanya. 33Farao Neko akamfunga kwa minyororo huko Ribla katika nchi ya Hamathi ili asiweze kutawala huko Yerusalemu, naye akatoza kodi ya talanta mia moja* za fedha, na talanta moja ya dhahabu* katika Yuda. 34Farao Neko akamfanya Eliakimu mwana wa Yosia kuwa mfalme mahali pa baba yake Yosia, na kulibadilisha jina la Eliakimu kuwa Yehoyakimu. Lakini akamchukua Yehoahazi na kumpeleka Misri, naye akafia huko.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.