Native Bible

2 Kings 23:1 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kisha mfalme akawaita pamoja wazee wote wa Yuda na Yerusalemu.

2 Kings 23:1 in English

2 Kings 23:1 · Berean Standard Bible

Then the king summoned all the elders of Judah and Jerusalem.

Context

1Kisha mfalme akawaita pamoja wazee wote wa Yuda na Yerusalemu. 2Akapanda kwenda hekaluni mwa Bwana pamoja na watu wa Yuda, watu wa Yerusalemu, makuhani na manabii, watu wote wakubwa kwa wadogo. Akasoma wakiwa wanasikia maneno yote ya Kitabu cha Agano, ambacho kilikuwa kimepatikana katika Hekalu la Bwana. 3Mfalme akasimama karibu na nguzo, na kufanya upya agano mbele za Bwana: yaani kumfuata Bwana na kuzishika amri zake, maagizo na sheria kwa moyo wake wote na kwa roho yake yote, hivyo kuyathibitisha maneno ya agano yaliyoandikwa katika kitabu hiki. Kisha watu wote wakajifunga wenyewe kwa kiapo katika agano.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.