2 Wafalme 2:5
2 Kings 2:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wana wa manabii waliokuwako huko Yeriko wakamwendea Elisha na kumuuliza, “Je, unajua ya kwamba Bwana atakuondolea bwana wako leo?” Akawajibu, “Ndiyo, najua, lakini msizungumze juu ya jambo hilo.”
2 Kings 2:5 in English
2 Kings 2:5 · Berean Standard Bible
Then the sons of the prophets at Jericho came up to Elisha and said, “Do you know that the LORD will take your master away from you today?” “Yes, I know,” he replied. “Do not speak of it.”
Context
3Wana wa manabii waliokuwako huko Betheli wakamjia Elisha na kumuuliza, “Je, unajua ya kwamba Bwana atakuondolea bwana wako leo?”
Elisha akawajibu, “Ndiyo, najua, lakini msizungumze juu ya jambo hilo.” 4Kisha Eliya akamwambia, “Baki hapa, Elisha. Bwana amenituma Yeriko.”
Naye akajibu, “Kwa hakika kama Bwana aishivyo na wewe uishivyo, sitakuacha.” Hivyo wakaenda Yeriko. 5Wana wa manabii waliokuwako huko Yeriko wakamwendea Elisha na kumuuliza, “Je, unajua ya kwamba Bwana atakuondolea bwana wako leo?”
Akawajibu, “Ndiyo, najua, lakini msizungumze juu ya jambo hilo.” 6Kisha Eliya akamwambia, “Kaa hapa. Bwana amenituma kwenda Yordani.”
Naye akamjibu, “Kwa hakika kama Bwana aishivyo na wewe uishivyo, sitakuacha.” Hivyo wote wawili wakaendelea pamoja. 7Wana hamsini wa manabii wakaenda na kusimama kwa mbali, kuelekea mahali ambapo Eliya na Elisha walikuwa wamesimama kando ya Mto Yordani.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.