2 Wafalme 19:34
2 Kings 19:34 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nitaulinda mji huu na kuuokoa, kwa ajili yangu mwenyewe, na kwa ajili ya Daudi mtumishi wangu.”
2 Kings 19:34 in English
2 Kings 19:34 · Berean Standard Bible
‘I will defend this city and save it for My own sake and for the sake of My servant David.’”
Context
32“Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana kuhusu mfalme wa Ashuru:
“Hataingia katika mji huu
wala hatapiga mshale hapa.
Hatakuja mbele yake akiwa na ngao,
wala kupanga majeshi kuuzingira. 33Kwa njia ile aliyoijia, ndiyo atakayorudi;
hataingia katika mji huu,
asema Bwana. 34Nitaulinda mji huu na kuuokoa,
kwa ajili yangu mwenyewe,
na kwa ajili ya Daudi mtumishi wangu.” 35Usiku ule, malaika wa Bwana akaenda, akawaua wanajeshi 185,000 katika kambi ya Waashuru. Wenzao walipoamka asubuhi yake, walikuta maiti kila mahali! 36Basi Senakeribu mfalme wa Ashuru akavunja kambi na kuondoka. Akarudi Ninawi na kukaa huko.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.