2 Wafalme 13:15
2 Kings 13:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Elisha akasema, “Leta upinde na baadhi ya mishale,” naye mfalme akafanya hivyo.
2 Kings 13:15 in English
2 Kings 13:15 · Berean Standard Bible
Elisha told him, “Take a bow and some arrows.” So Jehoash took a bow and some arrows.
Context
13Yehoashi akalala pamoja na baba zake, akazikwa Samaria pamoja na wafalme wa Israeli. Yeroboamu akawa mfalme baada yake. 14Wakati huu, Elisha alikuwa anaumwa na ugonjwa ambao baadaye ulimuua. Yehoashi mfalme wa Israeli akashuka kwenda kumwona na kumlilia. Akalia, “Baba yangu! Baba yangu! Magari ya vita ya Israeli na wapanda farasi wake!” 15Elisha akasema, “Leta upinde na baadhi ya mishale,” naye mfalme akafanya hivyo. 16Elisha akamwambia mfalme wa Israeli, “Shika upinde mikononi mwako.” Alipokwisha kuichukua, Elisha akaweka mikono yake juu ya mikono ya mfalme. 17Elisha akasema, “Fungua dirisha la mashariki,” naye akalifungua. Elisha akasema, “Piga mshale!” Naye akapiga mshale. Elisha akasema, “Mshale wa ushindi wa Bwana, mshale wa ushindi juu ya Aramu! Utawaangamiza Waaramu kabisa huko Afeki.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.