2 Wakorintho 8:13
2 Corinthians 8:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nia yetu si kwamba wengine wasaidike wakati ninyi mnateseka, bali pawe na uwiano.
2 Corinthians 8:13 in English
2 Corinthians 8:13 · Berean Standard Bible
It is not our intention that others may be relieved while you are burdened, but that there may be equality.
Context
11Sasa ikamilisheni kazi hii kwa shauku kama mlivyoanza, jitoleeni kulingana na uwezo wenu. 12Kwa kuwa kama nia ya kutoa ipo, kitolewacho kinakubalika kulingana na kile mtu alicho nacho, wala si kwa kile ambacho hana. 13Nia yetu si kwamba wengine wasaidike wakati ninyi mnateseka, bali pawe na uwiano. 14Kwa wakati huu, wingi wa vitu mlivyo navyo usaidie kutosheleza mahitaji yao, ili wakati wao watakapokuwa na wingi wa vitu, nao wapate kutosheleza mahitaji yenu. 15Ndipo patakuwa na usawa, kama ilivyoandikwa: “Aliyekusanya zaidi hakuwa na ziada, wala aliyekusanya kidogo hakupungukiwa.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.