Native Bible

2 Corinthians 12:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kwa habari ya jambo hili nilimsihi Bwana mara tatu aniondolee mwiba huu.

2 Corinthians 12:8 in English

2 Corinthians 12:8 · Berean Standard Bible

Three times I pleaded with the Lord to take it away from me.

Context

6Hata kama ningependa kujisifu, sitakuwa mjinga, kwa maana nitakuwa nasema kweli. Lakini najizuia, ili mtu yeyote asije akaniona mimi kuwa bora zaidi kuliko ninavyoonekana katika yale ninayotenda na kusema. 7Ili kunizuia nisijivune kwa sababu ya ufunuo huu mkuu, nilipewa mwiba katika mwili wangu, mjumbe wa Shetani, ili anitese. 8Kwa habari ya jambo hili nilimsihi Bwana mara tatu aniondolee mwiba huu. 9Lakini aliniambia, “Neema yangu inakutosha, kwa kuwa uweza wangu hukamilika katika udhaifu.” Kwa hiyo nitajisifu kwa furaha zaidi kuhusu udhaifu wangu, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu. 10Hii ndiyo sababu, kwa ajili ya Kristo, nafurahia udhaifu, katika kutukanwa, katika taabu, katika mateso na katika shida, kwa maana ninapokuwa dhaifu, ndipo nina nguvu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.