2 Wakorintho 10:17
2 Corinthians 10:17 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Lakini, “Yeye ajisifuye na ajisifu katika Bwana.”
2 Corinthians 10:17 in English
2 Corinthians 10:17 · Berean Standard Bible
Rather, “Let him who boasts boast in the Lord.”*
Context
15Wala hatuvuki mipaka kwa kujisifu kwetu kwa ajili ya kazi iliyofanywa na watu wengine. Tumaini letu ni kwamba imani yenu inavyozidi kukua, eneo letu la utendaji miongoni mwenu litapanuka zaidi, 16ili tuweze kuhubiri Injili sehemu zilizo mbali na maeneo yenu. Kwa maana hatutaki kujisifu kwa ajili ya kazi ambayo imekwisha kufanyika tayari katika eneo la mtu mwingine. 17Lakini, “Yeye ajisifuye na ajisifu katika Bwana.” 18Kwa maana si yeye ajisifuye mwenyewe akubaliwaye, bali yeye ambaye Bwana humsifu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.