2 Nyakati 25:2
2 Chronicles 25:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Akatenda yaliyo mema machoni pa Bwana, lakini sio kwa moyo wake wote.
2 Chronicles 25:2 in English
2 Chronicles 25:2 · Berean Standard Bible
And he did what was right in the eyes of the LORD, but not wholeheartedly.
Context
1Amazia alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu kwa miaka ishirini na tisa. Mama yake aliitwa Yehoadani kutoka Yerusalemu. 2Akatenda yaliyo mema machoni pa Bwana, lakini sio kwa moyo wake wote. 3Baada ya ufalme kuimarika mikononi mwake, aliwaua maafisa waliomuua mfalme baba yake. 4Hata hivyo hakuwaua watoto wao, lakini akafanya sawasawa na ilivyoandikwa katika Sheria, katika Kitabu cha Mose, ambako Bwana aliamuru: “Baba hawatauawa kwa ajili ya watoto wao, wala watoto hawatauawa kwa ajili ya baba zao. Kila mmoja atakufa kwa ajili ya dhambi zake mwenyewe.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.