Native Bible

2 Chronicles 15:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Wale wote ambao hawangemtafuta Bwana, Mungu wa Israeli wangelazimika kuuawa, akiwa mdogo au mkubwa, mwanaume au mwanamke.

2 Chronicles 15:13 in English

2 Chronicles 15:13 · Berean Standard Bible

And whoever would not seek the LORD, the God of Israel, would be put to death, whether young or old, man or woman.

Context

11Wakati huo wakamtolea Bwana dhabihu za ngʼombe 700, kondoo na mbuzi 7,000 kutoka zile nyara walizoteka. 12Wakafanya agano kumtafuta Bwana, Mungu wa baba zao kwa moyo wao wote na kwa roho yao yote. 13Wale wote ambao hawangemtafuta Bwana, Mungu wa Israeli wangelazimika kuuawa, akiwa mdogo au mkubwa, mwanaume au mwanamke. 14Wakamwapia Bwana kwa sauti kuu, kwa kupiga kelele, tarumbeta na kwa mabaragumu. 15Yuda wote wakafurahia kile kiapo kwa sababu walikuwa wameapa kwa moyo wao wote. Wakamtafuta Mungu kwa bidii, naye akaonekana kwao. Kwa hiyo Bwana akawastarehesha pande zote.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.