2 Nyakati 14:12
2 Chronicles 14:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Bwana akawapiga Wakushi mbele ya Asa na Yuda. Wakushi wakakimbia,
2 Chronicles 14:12 in English
2 Chronicles 14:12 · Berean Standard Bible
So the LORD struck down the Cushites before Asa and Judah, and the Cushites fled.
Context
10Asa akatoka kumkabili, nao wakapanga vita katika Bonde la Sefatha karibu na Maresha. 11Kisha Asa akamlilia Bwana Mungu wake na kusema, “Ee Bwana, hakuna yeyote aliye kama wewe wa kuwasaidia wasio na nguvu dhidi ya wenye nguvu. Utusaidie, Ee Bwana, wewe ndiwe Mungu wetu, kwa kuwa tunakutumainia wewe, nasi kwa jina lako tumekuja dhidi ya jeshi hili kubwa. Ee Bwana, wewe ndiwe Mungu wetu, usiwaache wanadamu wakushinde wewe.” 12Bwana akawapiga Wakushi mbele ya Asa na Yuda. Wakushi wakakimbia, 13naye Asa na jeshi lake wakawafuatia mpaka Gerari. Idadi kubwa ya Wakushi ilianguka hata wasiweze kuinuka tena, wakapondapondwa mbele za Bwana na majeshi yake. 14Watu wa Yuda wakachukua nyara nyingi sana, wakaangamiza vijiji vyote vinavyoizunguka Gerari, kwa kuwa hofu ya Bwana ilikuwa imewaangukia. Wakateka nyara vijiji hivi vyote, kwani kulikuwepo nyara nyingi huko.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.