1 Wathesalonike 1:7
1 Thessalonians 1:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hivyo ninyi mkawa kielelezo kwa waumini wote katika Makedonia na Akaya.
1 Thessalonians 1:7 in English
1 Thessalonians 1:7 · Berean Standard Bible
As a result, you have become an example to all the believers in Macedonia and Achaia.
Context
5kwa sababu ujumbe wetu wa Injili haukuja kwenu kwa maneno matupu bali pia ulidhihirishwa katika nguvu na katika Roho Mtakatifu, tena ukiwa na uthibitisho kamili, kama vile ninyi wenyewe mnavyojua jinsi tulivyoenenda katikati yenu kwa ajili yenu. 6Nanyi mkawa wafuasi wetu na wa Bwana, ingawa mlipata mateso mengi, mlilipokea lile Neno kwa furaha katika Roho Mtakatifu. 7Hivyo ninyi mkawa kielelezo kwa waumini wote katika Makedonia na Akaya. 8Kwa maana kutoka kwenu neno la Bwana limesikika, si katika Makedonia na Akaya tu, bali pia imani yenu katika Mungu imejulikana kila mahali kiasi kwamba hatuna haja ya kusema lolote kwa habari yake. 9Kwa maana watu wa maeneo hayo wenyewe wanaeleza jinsi mlivyotupokea na jinsi mlivyomgeukia Mungu mkaacha sanamu, ili kumtumikia Mungu aliye hai na wa kweli
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.