1 Samweli 8:9
1 Samuel 8:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Sasa wasikilize, lakini waonye kwa makini na uwafahamishe yale watakayotendewa na mfalme atakayewatawala.”
1 Samuel 8:9 in English
1 Samuel 8:9 · Berean Standard Bible
Now listen to them, but you must solemnly warn them and show them the manner of the king who will reign over them.”
Context
7Naye Bwana akamwambia: “Sikiliza yale yote watu wanakuambia. Si wewe ambaye wamekukataa, bali wamenikataa mimi kuwa mfalme wao. 8Kama vile walivyofanya tangu siku nilipowapandisha kutoka Misri mpaka siku hii ya leo; wakiniacha mimi na kutumikia miungu mingine, ndivyo wanavyokufanyia wewe. 9Sasa wasikilize, lakini waonye kwa makini na uwafahamishe yale watakayotendewa na mfalme atakayewatawala.” 10Samweli akawaambia wale watu waliokuwa wakiomba wapewe mfalme maneno yote ya Bwana. 11Akasema, “Hivi ndivyo atakavyowatendea mfalme atakayewatawala. Atawachukua wana wenu na kuwafanya watumike kwa magari yake ya vita na farasi, nao watakimbia mbele ya magari yake.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.