1 Samweli 8:13
1 Samuel 8:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Atawachukua binti zenu kuwa watengeneza manukato, wapishi na waokaji.
1 Samuel 8:13 in English
1 Samuel 8:13 · Berean Standard Bible
And he will take your daughters to be perfumers, cooks, and bakers.
Context
11Akasema, “Hivi ndivyo atakavyowatendea mfalme atakayewatawala. Atawachukua wana wenu na kuwafanya watumike kwa magari yake ya vita na farasi, nao watakimbia mbele ya magari yake. 12Baadhi yao atawaweka kuwa majemadari wa jeshi wa maelfu na majemadari wa jeshi wa hamsini, wengine kulima mashamba yake na kuvuna mavuno yake, pia na wengine kutengeneza silaha za vita na vifaa kwa ajili ya magari yake. 13Atawachukua binti zenu kuwa watengeneza manukato, wapishi na waokaji. 14Atayachukua mashamba yenu yaliyo mazuri, mashamba ya mizabibu na mashamba yenu ya mizeituni na kuwapa watumishi wake. 15Ataichukua sehemu ya kumi ya nafaka yenu na ya zabibu zenu na kuwapa maafisa wake na watumishi wake.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.