Native Bible

1 Samuel 26:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Hivyo Sauli akashuka kwenda katika Jangwa la Zifu, akiwa na watu wake 3,000 wa Israeli waliochaguliwa, kumsaka Daudi huko.

1 Samuel 26:2 in English

1 Samuel 26:2 · Berean Standard Bible

So Saul, accompanied by three thousand chosen men of Israel, went down to the Wilderness of Ziph to search for David there.

Context

1Hao Wazifu wakamwendea Sauli huko Gibea na kusema, “Je, Daudi hakujificha katika kilima cha Hakila, kinachotazamana na Yeshimoni?” 2Hivyo Sauli akashuka kwenda katika Jangwa la Zifu, akiwa na watu wake 3,000 wa Israeli waliochaguliwa, kumsaka Daudi huko. 3Sauli akapiga kambi yake kando ya barabara juu ya kilima cha Hakila kinachotazamana na Yeshimoni, lakini Daudi alikuwa anaishi huko jangwani. Alipoona kuwa Sauli amemfuata huko, 4Daudi akatuma wapelelezi na akapata habari kwa hakika kwamba Sauli alikuwa amewasili.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.