1 Samweli 18:14
1 Samuel 18:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Katika kila kitu alichofanya, Daudi alipata mafanikio makubwa, kwa sababu Bwana alikuwa pamoja naye.
1 Samuel 18:14 in English
1 Samuel 18:14 · Berean Standard Bible
and he continued to prosper in all his ways, because the LORD was with him.
Context
12Sauli akamwogopa Daudi, kwa sababu Bwana alikuwa pamoja na Daudi, lakini alikuwa amemwacha yeye. 13Kwa hiyo Sauli akamwondoa Daudi mbele yake na kumpa kuwa kiongozi wa watu elfu moja, naye Daudi akatoka na kuingia akiongoza vikosi katika vita. 14Katika kila kitu alichofanya, Daudi alipata mafanikio makubwa, kwa sababu Bwana alikuwa pamoja naye. 15Sauli alipoona jinsi alivyokuwa akifanikiwa, akamwogopa. 16Lakini Israeli wote na Yuda walimpenda Daudi, kwa sababu ndiye alikuwa akiwaongoza katika vita vyao.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.