1 Samweli 17:31
1 Samuel 17:31 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Lile Daudi alilosema likasikiwa na kuelezwa kwa Sauli, naye Sauli akatuma aitwe.
1 Samuel 17:31 in English
1 Samuel 17:31 · Berean Standard Bible
Now David’s words were overheard and reported to Saul, who called for him.
Context
29Daudi akasema, “Sasa nimefanya nini? Je, siwezi hata kuongea.” 30Daudi akamgeukia mtu mwingine na kumuuliza jambo lilo hilo, nao watu wakamjibu vilevile kama mwanzo. 31Lile Daudi alilosema likasikiwa na kuelezwa kwa Sauli, naye Sauli akatuma aitwe. 32Daudi akamwambia Sauli, “Mtu yeyote asife moyo kwa habari ya huyu Mfilisti; mtumishi wako atakwenda kupigana naye.” 33Sauli akamjibu Daudi, “Wewe hutaweza kwenda kupigana dhidi ya huyu Mfilisti; wewe ni kijana tu, naye amekuwa mtu wa vita tangu ujana wake.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.