1 Samweli 14:8
1 Samuel 14:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Yonathani akasema, “Basi njoo; tutavuka kuwaelekea hao watu na kuacha watuone.
1 Samuel 14:8 in English
1 Samuel 14:8 · Berean Standard Bible
“Very well,” said Jonathan, “we will cross over toward these men and show ourselves to them.
Context
6Yonathani akamwambia kijana wake mbeba silaha, “Njoo, tuvukie doria ya wale jamaa wasiotahiriwa. Huenda Bwana atatenda kwa ajili yetu. Hakuna chochote kitakachoweza kumzuia Bwana kuokoa, kwamba ni kwa wingi au kwa uchache.” 7Mbeba silaha wake akamwambia, “Fanya yale yote uliyo nayo katika moyo wako. Songa mbele; moyo wangu na roho yangu viko pamoja nawe.” 8Yonathani akasema, “Basi njoo; tutavuka kuwaelekea hao watu na kuacha watuone. 9Kama wakituambia, ‘Subirini hapo mpaka tuje kwenu,’ tutakaa pale tulipo na hatutakwea kwao. 10Lakini kama watasema, ‘Pandeni mje kwetu,’ tutakwea, kwa sababu hiyo itakuwa ishara yetu kwamba Bwana amewatia mikononi mwetu.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.