1 Samweli 14:42
1 Samuel 14:42 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Sauli akasema, “Pigeni kura kati yangu na mwanangu Yonathani.” Kura ikamwangukia Yonathani.
1 Samuel 14:42 in English
1 Samuel 14:42 · Berean Standard Bible
Then Saul said, “Cast the lot between me and my son Jonathan.” And Jonathan was selected.
Context
40Kisha Sauli akawaambia Waisraeli wote, “Ninyi simameni huko; mimi na mwanangu Yonathani tutasimama hapa.”
Watu wakajibu, “Fanya lile unaloona jema zaidi kwako.” 41Kisha Sauli akamwomba Bwana, Mungu wa Israeli, akisema, “Nipe jibu lililo sawa.” Yonathani na Sauli wakatolewa kwa kura, nao watu wakawa salama. 42Sauli akasema, “Pigeni kura kati yangu na mwanangu Yonathani.” Kura ikamwangukia Yonathani. 43Basi Sauli akamwambia Yonathani, “Niambie ni nini ulichokifanya.”
Hivyo Yonathani akamwambia, “Nilionja tu asali kidogo kwa ncha ya fimbo yangu. Je, sasa ni lazima nife?” 44Sauli akasema, “Mungu na anishughulikie kwa ukali zaidi kama wewe Yonathani hutakufa.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.