Native Bible

1 Peter 1:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Maana mnaupokea wokovu wa roho zenu, ambao ndio lengo la imani yenu.

1 Peter 1:9 in English

1 Peter 1:9 · Berean Standard Bible

now that you are receiving the goal of your faith, the salvation of your souls.

Context

7Haya yamewajia ili kwamba imani yenu, iliyo ya thamani kuliko dhahabu ipoteayo, ingawa hujaribiwa kwa moto, ionekane kuwa halisi na imalizie katika sifa, utukufu na heshima wakati Yesu Kristo atadhihirishwa. 8Ingawa hamjamwona, mnampenda; tena ingawa sasa hammwoni, mnamwamini na kujawa na furaha isiyoneneka yenye utukufu usioelezeka. 9Maana mnaupokea wokovu wa roho zenu, ambao ndio lengo la imani yenu. 10Kwa habari ya wokovu huu, wale manabii waliosema kuhusu neema ambayo ingewajia ninyi, walitafuta kwa bidii na kwa uangalifu mkubwa, 11wakijaribu kujua ni wakati upi na katika mazingira gani ambayo Roho wa Kristo aliyekuwa ndani yao alionyesha, alipotabiri kuhusu mateso ya Kristo na utukufu ule ambao ungefuata.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.