1 Wafalme 8:62
1 Kings 8:62 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kisha mfalme na Israeli wote pamoja naye wakatoa dhabihu mbele za Bwana.
1 Kings 8:62 in English
1 Kings 8:62 · Berean Standard Bible
Then the king and all Israel with him offered sacrifices before the LORD.
Context
60ili kwamba mataifa yote ya dunia wajue kwamba Bwana ndiye Mungu na kwamba hakuna mwingine. 61Lakini ni lazima mwiweke mioyo yenu kikamilifu kwa Bwana Mungu wetu, kuishi kwa maagizo yake na kutii amri zake, kama ilivyo wakati huu.” 62Kisha mfalme na Israeli wote pamoja naye wakatoa dhabihu mbele za Bwana. 63Solomoni akatoa dhabihu sadaka za amani kwa Bwana: ngʼombe 22,000, pamoja na kondoo na mbuzi 120,000. Hivyo ndivyo mfalme na Waisraeli wote walivyoweka wakfu Hekalu la Bwana. 64Siku iyo hiyo mfalme akaweka wakfu sehemu ya katikati ya ua uliokuwa mbele ya Hekalu la Bwana na hapo akatoa sadaka za kuteketezwa, sadaka za nafaka na mafuta ya sadaka za amani, kwa sababu madhabahu ya shaba iliyokuwa mbele za Bwana ilikuwa ndogo sana kuweza kubeba sadaka hizo za kuteketezwa, sadaka za nafaka na mafuta ya sadaka ya amani.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.