Native Bible

1 Kings 8:55 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Akasimama na kubariki kusanyiko lote la Israeli kwa sauti kubwa akisema:

1 Kings 8:55 in English

1 Kings 8:55 · Berean Standard Bible

And he stood and blessed the whole assembly of Israel in a loud voice, saying:

Context

53Kwa maana uliwachagua wao kutoka mataifa yote ya ulimwengu kuwa urithi wako mwenyewe, kama ulivyotangaza kupitia mtumishi wako Mose wakati wewe, Ee Bwana Mwenyezi, ulipowatoa baba zetu kutoka Misri.” 54Wakati Solomoni alipomaliza dua hizi zote na maombi kwa Bwana, akainuka kutoka mbele ya madhabahu ya Bwana, mahali alipokuwa amepiga magoti, mikono yake ikawa imekunjuliwa kuelekea juu mbinguni. 55Akasimama na kubariki kusanyiko lote la Israeli kwa sauti kubwa akisema: 56“Ahimidiwe Bwana, aliyewapa pumziko watu wake Israeli kama vile alivyokuwa ameahidi. Hakuna hata neno moja lililopunguka kati ya ahadi zote nzuri alizozitoa kupitia mtumishi wake Mose. 57Bwana Mungu wetu na awe pamoja nasi kama alivyokuwa na baba zetu, kamwe asituache wala kutukataa.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.