Native Bible

1 Kings 7:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Misingi iliwekwa kwa mawe makubwa yaliyo bora, yenye urefu wa dhiraa kumi* na mengine yenye urefu wa dhiraa nane*

1 Kings 7:10 in English

1 Kings 7:10 · Berean Standard Bible

The foundations were laid with large, costly stones, some ten cubits long * and some eight cubits long.*

Context

8Kwenye jumba la kifalme ambamo angeliishi, aliiweka nyuma zaidi, ikiwa na mjengo wa aina moja na hiyo nyingine. Pia Solomoni akajenga jumba la kifalme linalofanana na huo ukumbi mkubwa kwa ajili ya binti Farao, aliyekuwa amemwoa. 9Ujenzi huu wote, kuanzia nje mpaka kwenye ua mkuu na kuanzia kwenye msingi hadi upenuni, ulifanywa kwa mawe ya ubora wa hali ya juu yaliyokuwa yamechongwa kwa vipimo na kusawazishwa kwa msumeno nyuso zake za ndani na za nje. 10Misingi iliwekwa kwa mawe makubwa yaliyo bora, yenye urefu wa dhiraa kumi* na mengine yenye urefu wa dhiraa nane* 11Sehemu za juu kulikuwepo na mawe yenye ubora wa hali ya juu, yaliyokatwa kwa vipimo na boriti za mierezi. 12Ule ua mkuu ulizungukwa na ukuta wa safu tatu za mawe yaliyochongwa na safu moja ya boriti za mierezi zilizorembwa, kama ulivyokuwa ua wa ndani wa Hekalu la Bwana na baraza yake.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.