1 Wafalme 4:32
1 Kings 4:32 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Akanena mithali 3,000 na nyimbo zake zilikuwa 1,005.
1 Kings 4:32 in English
1 Kings 4:32 · Berean Standard Bible
Solomon composed three thousand proverbs, and his songs numbered a thousand and five.
Context
30Hekima ya Solomoni ilikuwa kubwa kuliko hekima ya watu wote wa Mashariki na kubwa kuliko hekima yote ya Misri. 31Alikuwa na hekima kuliko kila mwandishi, akiwemo Ethani Mwezrahi: kuliko Hemani, Kalkoli na Darda, wana wa Maholi. Umaarufu wake ukaenea kwa mataifa yote yaliyomzunguka. 32Akanena mithali 3,000 na nyimbo zake zilikuwa 1,005. 33Akaelezea maisha ya mimea kuanzia mwerezi wa Lebanoni hadi hisopo iotayo ukutani. Pia akafundisha kuhusu wanyama na ndege, wanyama wenye damu baridi, wakiwemo samaki. 34Watu wa mataifa yote wakaja kusikiliza hekima ya Solomoni, waliotumwa na wafalme wote wa ulimwengu, waliokuwa wamesikia juu ya hekima yake.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.