1 Wafalme 3:24
1 Kings 3:24 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kisha mfalme akasema, “Nileteeni upanga.” Basi wakamletea mfalme upanga.
1 Kings 3:24 in English
1 Kings 3:24 · Berean Standard Bible
The king continued, “Bring me a sword.” So they brought him a sword,
Context
22Huyo mwanamke mwingine akasema, “Hapana! Mwana aliye hai ndiye wangu, aliyekufa ni wako.”
Lakini yule wa kwanza akasisitiza, “Hapana! Mwana aliyekufa ni wako, aliye hai ni wangu.” Hivi ndivyo walivyobishana mbele ya mfalme. 23Mfalme akasema, “Huyu anasema, ‘Mwanangu ndiye aliye hai, na aliyekufa ndiye mwanao,’ maadamu yule anasema, ‘Hapana! Aliyekufa ni wako, na aliye hai ni wangu.’ ” 24Kisha mfalme akasema, “Nileteeni upanga.” Basi wakamletea mfalme upanga. 25Ndipo mfalme akatoa amri: “Mkate mtoto aliye hai vipande viwili; mpe huyu nusu na mwingine nusu.” 26Mwanamke ambaye mwanawe alikuwa hai akajawa na huruma kwa ajili ya mwanawe na kumwambia mfalme, “Tafadhali, bwana wangu, mpe yeye mtoto aliye hai! Usimuue!”
Lakini yule mwanamke mwingine akasema, “Mkate vipande viwili. Asiwe wangu au wake!”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.