1 Wafalme 22:38
1 Kings 22:38 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wakasafisha lile gari la vita katika bwawa la Samaria (mahali makahaba walipooga), na mbwa wakaramba damu yake, sawasawa na neno la Bwana lilivyokuwa limesema.
1 Kings 22:38 in English
1 Kings 22:38 · Berean Standard Bible
And the chariot was washed at the pool of Samaria where the prostitutes bathed,* and the dogs licked up Ahab’s blood, according to the word that the LORD had spoken.*
Context
36Jua lilipokuwa linazama, mbiu ikaenea katika jeshi lote: “Kila mtu aende mjini kwake, na kila mtu shambani kwake!” 37Basi mfalme akafa na akaletwa Samaria, nao wakamzika huko. 38Wakasafisha lile gari la vita katika bwawa la Samaria (mahali makahaba walipooga), na mbwa wakaramba damu yake, sawasawa na neno la Bwana lilivyokuwa limesema. 39Kwa matukio mengine ya utawala wa Ahabu, pamoja na yote aliyoyafanya, jumba la kifalme alilojenga na kupambwa kwa pembe za ndovu, nayo miji aliyoijengea maboma, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Israeli? 40Ahabu akalala pamoja na baba zake. Naye Ahazia mwanawe akawa mfalme baada yake.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.