1 Wafalme 19:7
1 Kings 19:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Yule malaika wa Bwana akaja tena mara ya pili, akamgusa akamwambia, “Inuka na ule, kwa kuwa safari ni ndefu kwako.”
1 Kings 19:7 in English
1 Kings 19:7 · Berean Standard Bible
A second time the angel of the LORD returned and touched him, saying, “Get up and eat, or the journey will be too much for you.”
Context
5Kisha akajinyoosha chini ya mti, akalala usingizi.
Mara malaika akamgusa na akamwambia, “Inuka na ule.” 6Akatazama pande zote, napo hapo karibu na kichwa chake palikuwepo mkate uliookwa kwenye makaa ya moto na gudulia la maji. Akala na kunywa, kisha akajinyoosha tena. 7Yule malaika wa Bwana akaja tena mara ya pili, akamgusa akamwambia, “Inuka na ule, kwa kuwa safari ni ndefu kwako.” 8Kwa hiyo akainuka, akala na kunywa. Akiwa ametiwa nguvu na kile chakula, akasafiri siku arobaini usiku na mchana mpaka akafika Horebu, mlima wa Mungu. 9Huko akaingia katika pango, akalala humo usiku ule.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.