1 Wafalme 18:35
1 Kings 18:35 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Maji yakatiririka kuizunguka madhabahu na hata kujaza lile handaki.
1 Kings 18:35 in English
1 Kings 18:35 · Berean Standard Bible
So the water ran down around the altar and even filled the trench.
Context
33Akapanga kuni, akamkata yule fahali vipande vipande na kuvipanga juu ya kuni. Kisha akawaambia, “Jazeni mapipa manne maji na kuyamwaga juu ya sadaka ya kuteketezwa na juu ya kuni.” 34Akawaambia, “Fanyeni hivyo tena.” Nao wakafanya hivyo tena.
Akaagiza, “Fanyeni kwa mara ya tatu.” Nao wakafanya hivyo kwa mara ya tatu. 35Maji yakatiririka kuizunguka madhabahu na hata kujaza lile handaki. 36Wakati wa kutoa dhabihu ya jioni, nabii Eliya akasogea mbele na kuomba, akisema: “Ee Bwana, Mungu wa Abrahamu, na Isaki na Israeli, ijulikane leo kwamba wewe ndiye Mungu katika Israeli na ya kwamba mimi ni mtumishi wako na nimefanya mambo haya yote kwa neno lako. 37Unijibu mimi, Ee Bwana, nijibu mimi, ili watu hawa wajue kwamba wewe, Ee Bwana, ndiwe Mungu, na kwamba unaigeuza mioyo yao ikurudie tena.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.