Native Bible

1 Kings 18:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Lakini sasa unaniambia niende kwa bwana wangu na kusema, ‘Eliya yuko hapa.’

1 Kings 18:11 in English

1 Kings 18:11 · Berean Standard Bible

And now you say, ‘Go tell your master that Elijah is here!’

Context

9Obadia akamuuliza, “Ni kosa gani nimefanya, hata ukaamua kumkabidhi mtumishi wako mkononi mwa Ahabu ili aniue? 10Hakika kama Bwana Mungu wako aishivyo, hakuna taifa hata moja au ufalme ambapo bwana wangu hajamtuma mtu kukutafuta. Kila wakati taifa au ufalme walipodai kwamba haupo huko, aliwafanya waape kwamba hawakuweza kukupata. 11Lakini sasa unaniambia niende kwa bwana wangu na kusema, ‘Eliya yuko hapa.’ 12Sijui ni wapi Roho wa Bwana ataamua kukupeleka wakati nitakapokuacha. Kama nikienda kumwambia Ahabu na asikupate, ataniua. Hata hivyo mimi mtumishi wako nimemwabudu Bwana tangu ujana wangu. 13Je, hukusikia, bwana wangu, nilifanya nini wakati Yezebeli alipokuwa akiua manabii wa Bwana? Niliwaficha manabii wa Bwana mia moja katika mapango mawili, hamsini katika kila moja, nami nikawapatia chakula na maji.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.