Native Bible

1 Kings 15:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Alitenda dhambi zote baba yake alizotenda kabla yake; moyo wake haukuwa mkamilifu kwa Bwana Mungu wake kama moyo wa Daudi baba yake ulivyokuwa.

1 Kings 15:3 in English

1 Kings 15:3 · Berean Standard Bible

And Abijam walked in all the sins that his father before him had committed, and his heart was not as fully devoted to the LORD his God as the heart of David his forefather had been.

Context

1Katika mwaka wa kumi na nane wa utawala wa Yeroboamu mwana wa Nebati, Abiya akawa mfalme wa Yuda, 2naye akatawala huko Yerusalemu miaka mitatu. Mama yake aliitwa Maaka binti Abishalomu.* 3Alitenda dhambi zote baba yake alizotenda kabla yake; moyo wake haukuwa mkamilifu kwa Bwana Mungu wake kama moyo wa Daudi baba yake ulivyokuwa. 4Pamoja na hayo, kwa ajili ya Daudi, Bwana Mungu wake akampa taa katika Yerusalemu kwa kumwinua mwana atawale badala yake na kwa kuifanya Yerusalemu kuwa imara. 5Kwa kuwa Daudi alifanya yaliyo mema machoni pa Bwana na hakushindwa kushika maagizo yote ya Bwana siku zote za uhai wake, isipokuwa katika habari ya Uria, Mhiti.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.