1 Wafalme 13:27
1 Kings 13:27 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nabii akawaambia wanawe, “Nitandikieni punda,” nao wakafanya hivyo.
1 Kings 13:27 in English
1 Kings 13:27 · Berean Standard Bible
Then the old prophet instructed his sons, “Saddle the donkey for me.” So they saddled it,
Context
25Baadhi ya watu waliopita pale waliona maiti imebwagwa pale chini, simba akiwa amesimama kando ya maiti, wakaenda na kutoa habari katika mji ambao nabii mzee aliishi. 26Yule nabii aliyekuwa amemrudisha kutoka safari yake aliposikia habari hii akasema, “Ni yule mtu wa Mungu ambaye aliasi neno la Bwana. Bwana amemtoa kwa simba, ambaye amemrarua na kumuua, sawasawa na neno la Bwana lilivyokuwa limemwonya.” 27Nabii akawaambia wanawe, “Nitandikieni punda,” nao wakafanya hivyo. 28Kisha akatoka akaenda akakuta maiti imebwagwa chini barabarani, punda na simba wakiwa wamesimama kando yake. Simba hakuwa amekula ile maiti wala kumrarua punda. 29Basi yule nabii mzee akachukua maiti ya mtu wa Mungu, akailaza juu ya punda na akairudisha katika mji wake, ili amwombolezee na kumzika.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.