1 Wafalme 11:30
1 Kings 11:30 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
naye Ahiya akachukua joho jipya alilokuwa amevaa akalirarua vipande kumi na viwili.
1 Kings 11:30 in English
1 Kings 11:30 · Berean Standard Bible
And Ahijah took hold of the new cloak he was wearing, tore it into twelve pieces,
Context
28Basi Yeroboamu alikuwa mtu shujaa na hodari, naye Solomoni alipoona jinsi kijana alivyofanya kazi yake, akamweka kuwa kiongozi wa kazi yote ya mikono ya nyumba ya Yosefu. 29Karibu na wakati ule Yeroboamu alikuwa anatoka nje ya Yerusalemu, Ahiya nabii Mshiloni akakutana naye njiani, akiwa amevaa joho jipya. Hawa wawili walikuwa peke yao mashambani, 30naye Ahiya akachukua joho jipya alilokuwa amevaa akalirarua vipande kumi na viwili. 31Kisha akamwambia Yeroboamu, “Chukua vipande kumi kwa ajili yako, kwa kuwa hivi ndivyo Bwana, Mungu wa Israeli asemavyo: ‘Tazama, ninakwenda kuuchana ufalme kutoka mikononi mwa Solomoni na kukupa wewe makabila kumi. 32Lakini kwa ajili ya mtumishi wangu Daudi na mji wa Yerusalemu, ambao nimeuchagua miongoni mwa makabila yote ya Israeli, atakuwa na kabila moja.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.