Native Bible

1 Kings 10:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Uzito wa dhahabu ambayo Solomoni alipokea kwa mwaka ulikuwa talanta 666,*

1 Kings 10:14 in English

1 Kings 10:14 · Berean Standard Bible

The weight of gold that came to Solomon each year was 666 talents,*

Context

12Mfalme akatumia miti ya msandali kuwa nguzo ya Hekalu la Bwana na kwa jumba la kifalme, pia kwa kutengeneza vinubi na zeze kwa ajili ya waimbaji. Kiasi hicho kingi cha msandali hakijawahi kuingizwa au kuonekana humo tangu siku ile.) 13Mfalme Solomoni akampa malkia wa Sheba kila kitu alichotamani na kukiomba, kando na vile mfalme alivyokuwa amempa kwa ukarimu wake wa kifalme. Kisha malkia akaondoka na kurudi katika nchi yake, yeye na watumishi wake. 14Uzito wa dhahabu ambayo Solomoni alipokea kwa mwaka ulikuwa talanta 666,* 15mbali na mapato kutoka kwa wafanyabiashara na wachuuzi, na kutoka kwa wafalme wote wa Kiarabu na watawala wa nchi. 16Mfalme Solomoni akatengeneza ngao kubwa 200 kwa dhahabu iliyofuliwa; kila ngao ilikuwa na dhahabu yenye uzito wa shekeli 600*

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.