1 Yohana 5:2
1 John 5:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hivi ndivyo tunavyojua kwamba tunawapenda watoto wa Mungu, kwa kumpenda Mungu na kuzitii amri zake.
1 John 5:2 in English
1 John 5:2 · Berean Standard Bible
By this we know that we love the children of God: when we love God and keep His commandments.
Context
1Kila mtu anayeamini kwamba Yesu ndiye Kristo amezaliwa na Mungu, na yeyote ampendaye Baba humpenda pia mtoto aliyezaliwa naye. 2Hivi ndivyo tunavyojua kwamba tunawapenda watoto wa Mungu, kwa kumpenda Mungu na kuzitii amri zake. 3Huku ndiko kumpenda Mungu, yaani, kuzitii amri zake. Nazo amri zake si nzito. 4Kwa maana kila aliyezaliwa na Mungu huushinda ulimwengu. Huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, yaani, hiyo imani yetu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.