Native Bible

1 John 4:19 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Twampenda yeye kwa sababu yeye alitupenda kwanza.

1 John 4:19 in English

1 John 4:19 · Berean Standard Bible

We love * because He first loved us.

Context

17Kwa njia hii, pendo hukamilishwa miongoni mwetu ili tupate kuwa na ujasiri katika siku ya hukumu, kwa sababu kama alivyo ndivyo tulivyo sisi katika ulimwengu huu. 18Katika pendo hakuna hofu. Lakini pendo lililo kamili huitupa nje hofu, kwa sababu hofu inahusika na adhabu. Kila mwenye hofu hakukamilika katika pendo. 19Twampenda yeye kwa sababu yeye alitupenda kwanza. 20Ikiwa mtu atasema, “Nampenda Mungu,” lakini anamchukia ndugu yake, yeye ni mwongo. Kwa maana kila mtu asiyempenda ndugu yake ambaye anamwona, atampendaje Mungu asiyemuona? 21Naye ametupa amri hii: Yeyote anayempenda Mungu lazima pia ampende ndugu yake.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.