1 Yohana 1:6
1 John 1:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kama tukisema kwamba twashirikiana naye huku tukienenda gizani, twasema uongo, wala hatutendi lililo kweli.
1 John 1:6 in English
1 John 1:6 · Berean Standard Bible
If we say we have fellowship with Him yet walk in the darkness, we lie and do not practice the truth.
Context
4Tunaandika mambo haya ili furaha yetu ipate kuwa timilifu. 5Huu ndio ujumbe tuliosikia kutoka kwake na kuwatangazia ninyi: kwamba Mungu ni nuru na ndani yake hamna giza lolote. 6Kama tukisema kwamba twashirikiana naye huku tukienenda gizani, twasema uongo, wala hatutendi lililo kweli. 7Lakini tukienenda nuruni, kama yeye alivyo nuruni, twashirikiana sisi kwa sisi na damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote. 8Kama tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe wala kweli haimo ndani yetu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.