Native Bible

1 Corinthians 9:23 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Nafanya haya yote kwa ajili ya Injili, ili nipate kushiriki baraka zake.

1 Corinthians 9:23 in English

1 Corinthians 9:23 · Berean Standard Bible

I do all this for the sake of the gospel, so that I may share in its blessings.

Context

21Kwa watu wasio na sheria nilikuwa kama asiye na sheria (ingawa siko huru mbali na sheria ya Mungu, bali niko chini ya sheria ya Kristo), ili niweze kuwapata wale wasio na sheria. 22Kwa walio dhaifu nilikuwa dhaifu, ili niweze kuwapata walio dhaifu. Nimekuwa mtu wa hali zote kwa watu wote ili kwa njia yoyote niweze kuwaokoa baadhi yao. 23Nafanya haya yote kwa ajili ya Injili, ili nipate kushiriki baraka zake. 24Je, hamjui kwamba katika mashindano ya mbio wote wanaoshindana hukimbia, lakini ni mmoja wao tu apewaye tuzo? Kwa hiyo kimbieni katika mashindano kwa jinsi ambavyo mtapata tuzo. 25Kila mmoja anayeshiriki katika mashindano hufanya mazoezi makali. Wao hufanya hivyo ili wapokee taji isiyodumu, lakini sisi tunafanya hivyo ili kupata taji idumuyo milele.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.