1 Wakorintho 15:25
1 Corinthians 15:25 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa maana lazima Kristo atawale mpaka awe amewaweka adui zake wote chini ya miguu yake.
1 Corinthians 15:25 in English
1 Corinthians 15:25 · Berean Standard Bible
For He must reign until He has put all His enemies under His feet.
Context
23Lakini kila mmoja kwa wakati wake: Kristo, tunda la kwanza kisha, wale walio wake, wakati atakapokuja. 24Ndipo mwisho utafika, wakati atakapomkabidhi Mungu Baba ufalme, akiisha angamiza kila utawala na kila mamlaka na nguvu. 25Kwa maana lazima Kristo atawale mpaka awe amewaweka adui zake wote chini ya miguu yake. 26Adui wa mwisho atakayeangamizwa ni mauti. 27Kwa maana Mungu “ameweka vitu vyote chini ya miguu yake.” Lakini isemapo kwamba “vitu vyote” vimewekwa chini yake, ni wazi kwamba Mungu aliyetiisha vitu vyote chini ya Kristo hayumo miongoni mwa hivyo vilivyotiishwa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.