Native Bible

1 Corinthians 15:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Lakini kama hakuna ufufuo wa wafu, basi hata Kristo hakufufuliwa.

1 Corinthians 15:13 in English

1 Corinthians 15:13 · Berean Standard Bible

If there is no resurrection of the dead, then not even Christ has been raised.

Context

11Hivyo basi, kama ilikuwa mimi au wao, hili ndilo tunalohubiri, na hili ndilo mliloamini. 12Basi kama tumehubiri ya kwamba Kristo alifufuliwa kutoka kwa wafu, mbona baadhi yenu mnasema hakuna ufufuo wa wafu? 13Lakini kama hakuna ufufuo wa wafu, basi hata Kristo hakufufuliwa. 14Tena ikiwa Kristo hakufufuliwa kutoka kwa wafu, kuhubiri kwetu kumekuwa ni bure na imani yenu ni batili. 15Zaidi ya hayo, twaonekana kuwa mashahidi wa uongo kuhusu Mungu, kwa sababu tumeshuhudia kumhusu Mungu kwamba alimfufua Kristo kutoka kwa wafu, lakini hilo haliwezi kuwa kweli kama wafu hawafufuliwi.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.