1 Wakorintho 1:21
1 Corinthians 1:21 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa kuwa katika hekima ya Mungu, ulimwengu kwa hekima yake haukumjua yeye, ilimpendeza Mungu kuwaokoa wale walioamini kwa upuzi wa lile neno lililohubiriwa.
1 Corinthians 1:21 in English
1 Corinthians 1:21 · Berean Standard Bible
For since in the wisdom of God the world through its wisdom did not know Him, God was pleased through the foolishness of what was preached to save those who believe.
Context
19Kwa maana imeandikwa:
“Nitaiharibu hekima ya wenye hekima,
na kubatilisha akili ya wenye akili.” 20Yuko wapi mwenye hekima? Yuko wapi msomi? Yuko wapi mwanafalsafa wa nyakati hizi? Je, Mungu hakufanya hekima ya ulimwengu huu kuwa upumbavu? 21Kwa kuwa katika hekima ya Mungu, ulimwengu kwa hekima yake haukumjua yeye, ilimpendeza Mungu kuwaokoa wale walioamini kwa upuzi wa lile neno lililohubiriwa. 22Wayahudi wanadai ishara za miujiza na Wayunani wanatafuta hekima. 23Lakini sisi tunamhubiri Kristo aliyesulubiwa: yeye kwa Wayahudi ni kikwazo na kwa Wayunani ni upuzi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.