1 Nyakati 25:3
1 Chronicles 25:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wana wa Yeduthuni walikuwa sita: Gedalia, Seri, Yeshaya, Shimei, Hashabia, na Matithia, nao walikuwa chini ya usimamizi wa baba yao Yeduthuni, wao walikuwa wakitoa unabii wakitumia vinubi, wakimshukuru na kumtukuza Bwana.
1 Chronicles 25:3 in English
1 Chronicles 25:3 · Berean Standard Bible
From the sons of Jeduthun: Gedaliah, Zeri, Jeshaiah, Shimei,* Hashabiah, and Mattithiah—six in all—under the direction of their father Jeduthun, who prophesied with the harp, giving thanks and praise to the LORD.
Context
1Daudi, pamoja na majemadari wa jeshi, wakawatenga baadhi ya wana wa Asafu, wana wa Hemani na wana wa Yeduthuni, kwa ajili ya huduma ya kutoa unabii, wakitumia vinubi, zeze na matoazi. Hii ndiyo orodha ya watu waliofanya huduma hii: 2Kutoka kwa wana wa Asafu walikuwa:
Zakuri, Yosefu, Nethania na Asarela. Wana wa Asafu walikuwa chini ya usimamizi wa Asafu, ambaye alitoa unabii chini ya usimamizi wa mfalme. 3Wana wa Yeduthuni walikuwa sita:
Gedalia, Seri, Yeshaya, Shimei, Hashabia, na Matithia, nao walikuwa chini ya usimamizi wa baba yao Yeduthuni, wao walikuwa wakitoa unabii wakitumia vinubi, wakimshukuru na kumtukuza Bwana. 4Wana wa Hemani walikuwa:
Bukia, Matania, Uzieli, Shebueli na Yeremothi, Hanania, Hanani, Eliatha, Gidalti na Romamti-Ezeri, Yoshbekasha, Malothi, Hothiri na Mahaziothi. 5Wote hawa walikuwa wana wa Hemani mwonaji wa mfalme. Aliwapata wana hawa kutokana na ahadi ya Mungu ili kumwinua. Mungu alimpa Hemani wana kumi na wanne na binti watatu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.