1 Nyakati 15:13
1 Chronicles 15:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ilikuwa ni kwa sababu hii, ninyi Walawi, hamkulipandisha Sanduku la Bwana mara ya kwanza, hata ikasababisha Bwana Mungu wetu kuwaka hasira dhidi yetu. Hatukumuuliza jinsi ya kufanya ili tupate kulileta jinsi alivyoagiza.”
1 Chronicles 15:13 in English
1 Chronicles 15:13 · Berean Standard Bible
It was because you Levites were not with us the first time that the LORD our God burst forth in anger against us. For we did not consult Him about the proper order.”
Context
11Kisha Daudi akawaita makuhani Sadoki na Abiathari, pamoja na Walawi Urieli, Asaya, Yoeli, Shemaya, Elieli na Aminadabu. 12Akawaambia, “Ninyi ndio viongozi wa jamaa za Walawi. Ninyi pamoja na Walawi wenzenu inawapasa mjitakase na kulipandisha Sanduku la Bwana, Mungu wa Israeli hadi mahali ambapo nimetengeneza kwa ajili yake. 13Ilikuwa ni kwa sababu hii, ninyi Walawi, hamkulipandisha Sanduku la Bwana mara ya kwanza, hata ikasababisha Bwana Mungu wetu kuwaka hasira dhidi yetu. Hatukumuuliza jinsi ya kufanya ili tupate kulileta jinsi alivyoagiza.” 14Kwa hiyo makuhani pamoja na Walawi wakajitakasa ili kulipandisha Sanduku la Bwana, Mungu wa Israeli. 15Nao Walawi wakalichukua Sanduku la Mungu mabegani mwao wakitumia mipiko, kama vile Mose alivyoamuru sawasawa na neno la Bwana.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.