1 Nyakati 13:1
1 Chronicles 13:1 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Daudi alishauriana na kila afisa wake, majemadari wa maelfu na majemadari wa mamia.
1 Chronicles 13:1 in English
1 Chronicles 13:1 · Berean Standard Bible
Then David conferred with all his leaders, the commanders of hundreds and of thousands.
Context
1Daudi alishauriana na kila afisa wake, majemadari wa maelfu na majemadari wa mamia. 2Ndipo Daudi akaliambia kusanyiko lote la Israeli, “Kama mkiona ni vyema, na kama ni mapenzi ya Bwana Mungu wetu, tupeleke ujumbe kwa ndugu zetu wengine walio mbali na walio karibu katika nchi yote ya Israeli, pia kwa makuhani na Walawi walio pamoja nao katika miji yao na katika sehemu zao za malisho yao, waje waungane na sisi. 3Sisi na tulirudishe Sanduku la Mungu wetu kwetu kwa maana hatukujali wakati wa utawala wa Sauli.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.